KIBONDE AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA HOTUBA YENYE KUIMARISHA UTULIVU

 


Na mwandishi wetu

MWENYEKITI wa Chama Cha Makini Taifa, Coaster Kibonde,amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa hotuba yake iliyojaa ukoma na weledi aliyoitoa mbele ya wazee wa Jiji la Dar es Salaam.Kibonde amesema hotuba imeonyesha ujasiri mkubwa na ni ya mfano kwani imeweka  sura ya nchi kwamba ina kiongozi shupavu na jasiri mwenye dhamira ya kulinda amani na utulivu wa Taifa.

Akizungumza na mwandishi kwa mahojiano maalum amesema kwamba ameonyesha  sauti ya mamlaka ya kwamba Tanzania inaendeshwa kwa mujibu wa Sheria haiwezi kuingiliwa na nchi nyingine yoyote.

Aidha,Kibonde alisema kwamba ni muhimu kwa wananchi kuheshimu maagizo ya mamlaka zilizopo kwa manufaa ya  Taifa.

"Hakuna kiongozi anayetamani wananchi wake wapate shida .Kila kiongozi mwenye busara hutaka kuona watu wake wakiishi kwa furaha,amani, upendo na utulivu",alisema 

Pia amewataka vijana nchini kuendelea kudumisha amani na kutii Sheria hasa kipindi hiki kinapoelekea tarehe 9 Desemba.

Sanjari na hayo,Amesema kwamba viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kulinda na kutetea amani,hivyo vijana wanatakiwa kusikiliza maongozi ya kirohi yanayojenga jamii tulivu.

Post a Comment

Previous Post Next Post