KIBONDE AWATAKA WATANZANIA KUSHEREHEKEA SIKU YA UHURU KWA AMANI

 

Na mwandishi wetu

MWENYEKITI Taifa wa Chama cha Makini, Coaster Kibonde anawatakia watanzania wote kusherehekea kwa Amani sherehe za Uhuru  inayoazimishwa Kila mwaka Desemba 9.

Hayo yamebainishwa Leo Desemba 8,2025 Katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama Mabibo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza kwa mahojiano na maalum ambapo Mwenyekiti Kibonde amewaomba watanzania kutumia siku hiyo kujenga umoja,mshikamano na kudumisha amani ya nchi yetu.

Aidha,amewataka watanzania kujiepusha na mihemko ya watu wanaochochea vurugu wasiolitakia mema Taifa letu kuwapuuza kwani hawana Nia njema.

Pia amewataka vijana kuepukana Wala kutokubali kuyumbishwa kwa namna Moja au nyingine  na watu wenye dhamira ovu kwa nchi yetu kwani serikali imesikia kilio Cha vijana na kwamba imeanzisha wizara maalum ,hivyo vijana wanatakiwa kupeleka hoja zao ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.

"Amesisitiza kwamba watanzania tuilinde amani ya nchi yetu ambayo tumeirithi kutoka kwa waasisi wetu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume,tuidumishe ,tuienzi ili Taifa letu liendelee kuwa kimbilio la wengi",alisema Kibonde

Hata hivyo amesema tutumie siku hiyo ya Desemba 9,kupumzika majumbani Kwa wale ambao hawana umuhimu wa kutoka na wale watakaotoka watoke kwa ajili ya kwenda kutafuta kipato cha siku ili kuhudumia familia zao nao pia waendelee kudumisha amani kujiepusha na vitendo vinavyoleta uvunjifu wa amani

Aliendelea kwa kusema kuwa vijana  maendeleo ya nchi yetu yataletwa na vijana kwa ushiriki wao katika kujenga uchumi shirikishi mfano kama Marekani Rais aliyepo madarakani ni wa awamu ya 47 hivyo hatuwezi kulingana na Tanzania ikiwa Rais aliyepo ni wa awamu ya Sita hivyo kimaendeleo watakuwa wamepiga hatua ,kwahiyo watanzania tuendelee kudumisha amani ya Taifa letu kwani maendeleo ya Tanzania yataletwa na watanzania wenyewe tukiwa wamoja.

Post a Comment

Previous Post Next Post