Na mwandishi wetu
Dar es Salaam
MCHUNGAJI wa Kanisa la Tanzania Assembles of God(TAG) Mwanagati,Zabron Mwizagi ametoa wito kwa wananchi kujilinda na mambo mabaya yasiyompendeza Mungu hasa katika kipindi hiki tunapoelekea katika sikukuu za Krismas na mwaka mpya .
Akizungumza na waandishi wa habari Leo Desemba 15,2025 Jijini Dar es Salaam amesema kuwa tunaelekea katika kipindi cha sikukuu za Krismas tunapaswa kuwa watulivu tunapongoja siku ya kuzaliwa Mwokozi ni siku kubwa ambayo inatukumbusha kuzaliwa Mwokozi wetu.
Aidha,amesema kwamba 2025/2026 ni kipindi cha kupendana na kukaribishana na kuendeleleza umoja wetu wa Kitaifa,tuwe na umoja na amani ndio jambo muhimu na la msingi kwa nchi yetu na Taifa
"Tusiondoe umoja wetu na kitaifa ,tuwe na umoja na Amani ,kwani ni jambo la msingi sana ,nalitakia amani Taifa letu na nchi yetu,sikukuu ya Krismas na mwaka mpya ziwe za amani na utulivu,alisema Mchungaji Mwizagi
Pia amesema tatizo la maadili limekuwa kubwa kutokana na utandawazi ,teknolojia imekuwa duniani hivyo kupelekea mmomonyoko wa maadili kuongezeka, tunatakiwa kuyatazama na kuwafundisha vijana kuwa na hofu ya Mungu ili waweze kuepukana na maovu
Alimalizia kwa kuwatakia sikukuu njema za kumaliza mwaka
