TANFORD YATOA FURSA KWA WAJASIRIAMALI NA WAFANYABIASHARA

 

Na mwandishi wetu

MWENYEKITI wa Umoja wa Wafanyabiashara wasafirishaji wa Mizigo toka Dubai ,Hussein Jamal amewataka watanzania kuchangamkia fursa muhimu ya kushiriki kwenye kongamano la Tanzania Trade and Logistic Forum 2026(TANFORD).

Akizungumza na waandishi wa habari Leo Desemba 16,2025 Jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti Jamal amesema kongamano Hilo litafanyika Februari 13-14,2026 Dubai na litakuwa na fursa kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wa Tanzania ambao watakutana na wenzao kutoka sehemu mbalimbali duniani na litawafungua kimawazo na kifikra na kufika mbali kwenye biashara zao

"Forum imepata uthibitisho na ushirikiano rasmi kutoka Ubalozi wa Tanzania - UAE, na inalenga kuunga mkono juhudi za taifa katika kuvutia uwekezaji, kukuza biashara na kuimarisha nafasi ya Tanzania kama kitovu cha biashara na lojistiki Afrika Mashariki", alisema

Hata hivyo ,amesema dhumuni Kuu la Kongamano TTLF 2026 inalenga (a) Kukuza biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na UAE/GCC kuleta wawekezaji wakubwa, taasisi za kifedha, makampuni ya masoko na wazalishaji ili kujua fursa za Tanzania.

a) Kutangaza fursa zilizopo Tanzania ikiwa ni pamoja na TPA, TRC, TAA, TANTRADE, TISEZA, ZIPA na taasisi nyingine za serikali na Binafasi

(c) Kujenga majukwaa ya ushirikiano kati ya sekta binafsi na serikali kwa ajili ya mikataba, ubia, na ujenzi wa miradi ya kimkakati.

(d) Kuunga mkono makampuni ya cargo, clearing & forwarding, na logistics kwa kuyakutanisha na masoko mapya ya UAE, GCC na Asia

(e) Kupanua fursa kwa vijana kupitia Youth Innovation & Business Stage ambapo vijana wenye mawazo ya biashara watapata nafasi ya kuwasilisha miradi yao mbele ya wawekezaji.

Sanjari na hayo amesema kwamba Malengo Mahususi ni Kuongeza uwekezaji wa moja kwa moja (FDI) kutoka UAE kwenda Tanzania pamoja  na kusaidia makampuni ya Tanzania kupenya katika soko la kimataifa

Aliongeza kwamba pia Kujenga mitandao ya biashara yenye tija na  Kufungua milango ya ushirikiano kwa nchi zisizo na bandari zinazotumia Tanzania kama lango la biashara

Aliendelea kwamba kuboresha taswira ya Tanzania kama kitovu cha biashara, utalii na uchumi wa viwanda na washiriki wanatarajiwa ni taasisi za serikali ya Tanzania na makampuni ya sekta binafsi kutoka Tanzania na Makampuni kutoka UAE, GCC, Asia & Afrika ,Taasisi za kifedha, Wawekezaji wakubwa na wawekezaji binafsi

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TATOA Elias Lukumay amewataka vijana kuchangamkia fursa hii ili kukuza biashara zao na kuongeza ufanisi.

Naye Rais wa Tanzania Fraught Forward Association ( TAFA) Edward Urio amesema kongamano Hilo Lina umuhimu mkubwa katika sekta ya usafirishaji wa mizigo na ni fursa kwa nchi zisizo na bandari na zinazotumia bandari ya Dar es Salaam 

TANFORD ni jukwaa rasmi la kuratibu, kuunganisha na kuwakilisha Watanzania wanaofanya biashara za cargo, logistics na trade ndani ya UAE, kwa lengo la kukuza biashara na ushirikiano kati ya Tanzania na Dubai

Post a Comment

Previous Post Next Post