WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema Mpango wa Elimu kwa Umma Kuhusu Muungano utakuwa endelevu ili kuhakikisha elimu hiyo inawafikia kila mmoja
Ameyasema hayo Desemba 19,2025 wakati akizungumza katika kipindi Cha Asubuhi kinachorushwa na ZBC ambapo amesema waandishi wa habari wanayo nafasi kubwa katika utoaji wa elimu kwa umma ndio maana Ofisi ya Makamu wa Rais imewapa nafasi na itakuwa ikishirikiana nao kwa asilimia kubwa
"Katika kuhakikisha Hilo Leo tumeandaa semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari Zanzibar Kisha tutafanya kwa Wahariri Bara na baadaye tutaandaa makongamano mbalimbali",
Amesema Mpango wa Elimu kwa Umma kuhusu Muungano wanufaika wakubwa watakuwa vijana ambao ndio walengwa kutokana na wengi wao kuwa wamemaliza baada ya Muungano(1964)
