DKT. SAMIA AIPA TAIFA STARS SHILINGI MILIONI 500

 


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameipatia Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) zawadi ya shilingi milioni 500 kufuatia kufanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora katika michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) inayoendelea nchini Morocco 🇲🇦.

Taarifa hiyo imetolewa leo, Januari 03, 2026, na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, alipowasiliana na wachezaji pamoja na benchi la ufundi la Taifa Stars kwa njia ya simu, kupitia Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda.

Rais Dkt. Samia amepongeza wachezaji, benchi la ufundi na Watanzania wote kwa mafanikio hayo ya kihistoria, huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono Taifa Stars katika safari yao ya kupeperusha bendera ya Taifa.

Post a Comment

Previous Post Next Post