JESHI LA POLISI DAR LATHIBITISHA AJALI YA MAGARI KADHAA BARABARA YA MOROCCO ,KINONDONI

 


Na Mwandishi wetu

DAR ES SALAAM

JESHI  la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kutokea kwa ajali ya barabarani iliyohusikia magari kadhaa kugongana katika Barabara ya Bagamoyo, eneo la Morocco, Wilaya ya Kinondoni.

Ajali hiyo imetokea tarehe 20 Januari 2026 majira ya saa 5:20 usiku, ikihusisha gari lenye namba za usajili T 491 EGT aina ya Subaru Forester, lililokuwa likiendeshwa na Paschal Emanuel, mkazi wa Goba, Ubungo, Dar es Salaam.

Taarifa zinaeleza kuwa dereva huyo alikuwa akitokea eneo la Victoria kuelekea Morocco, ambapo aligonga kwa nyuma gari lenye namba T 847 DKR aina ya Toyota Prado, lililokuwa likiendeshwa na Salumu Mwalimu, mkazi wa Kinondoni, Dar es Salaam.

Baada ya tukio hilo, gari la Subaru Forester lilipoteza mwelekeo, likagonga kingo za barabara kabla ya kuingia katika eneo la kampuni ya Car Point, linalohifadhi magari yanayosubiri kuuzwa, na kugonga magari mengine matatu yaliyokuwa yameegeshwa hapo.

Katika ajali hiyo, Moza Ally, mkazi wa Kinondoni, alipata majeraha na kukimbizwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) kwa matibabu, ambapo aliruhusiwa baada ya kupata huduma za kitabibu.

Jeshi la Polisi limethibitisha kuwa dereva wa gari la Subaru Forester, T 491 EGT, anashikiliwa kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

Aidha, Polisi wametoa wito kwa watumiaji wote wa barabara, wakiwemo waendesha vyombo vya moto, kuendelea kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani ili kuzuia na kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.

Post a Comment

Previous Post Next Post