Na Mwandishi wetu
DAR ES SALAAM
MTUMISHI wa Mungu Nabii Edmond Mystic wa Kanisa la Heaven Image Manifest amewataka vijana nchini kusimama kama wazawa wa nchi hii ya Tanzania kutangaza amani na haki katika Taifa.
Hayo yamebainishwa na mtumishi Mystic jijini Dar es Salaam muda mchache kabla ya Mkesha wa Usiku wa kutiwa alama ya Mgeuko uliofanyika katika Viwanja vya Kenton Sinza Afrikasana Jijini Dar es Salaam.
Aidha,amesema mkesha huo umeandaliwa kwa lengo la kuwakutanisha watu mabalimbali ili kuvuka mwaka mpya pamoja,kwa kumtazama Mungu kama msingi wa mabadiliko ya kimwili na kiroho katika maisha ya mwanadamu.
Nabii Mystic amesema maisha ya Majira mbalimbali na kila majira mapya yanabeba aina Fulani ya mambo mapya ,kwa hiyo tunapaswa kutokubali kuishi katika majira yaliyopita bali kuishi kwa kusudi la Mungu.
Pia ametoa wito kwa watanzania kushiriki Ibada na kuwapeleka watu wenye matatizo mbalimbali ya kiafya wakaombewe na kupokea uponyaji
Aliendelea kwamba si kweli kwamba mwaka mpya huwa mpya kwa kila mtu,bali mwaka mpya huwa mpya pale mtu anaposhuhudia mabadiliko mapya yanapotokea katika maisha ya mtu.
