WAZIRI MKUU KUMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA KATIKA MAZISHI YA MZEE EDWIN MTEI

 


WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Januari 24, 2026, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ambapo anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika mazishi ya marehemu Mzee Edwin Mtei, yanayofanyika Tengeru, jijini Arusha.

Mzee Edwin Mtei, ambaye aliwahi kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuanzia mwaka 1966 hadi 1974, alifariki dunia usiku wa Januari 19, 2026, jijini Arusha.




Post a Comment

Previous Post Next Post