BIMA YA AFYA KWA WOTE INALENGA MAKUNDI MAALUM YA KIMKAKATI

 

Na Mwandishi wetu

WAZIRI wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema mpango wa Bima ya Afya kwa Wote umejikita kuyafikia makundi maalum ya kimkakati ikiwemo wafugaji, wakulima, wasanii, waendesha bodaboda na wachimbaji wadogo.

Waziri Mchengerwa ameyasema hayo Februari 2, 2026, wakati akizungumza katika kikao kazi na wahariri wa vyombo vya habari kilichofanyika Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam.

Waziri Mchengerwa amesema dhamira kuu ya Serikali ni kumfuata mwananchi popote alipo kwa kutumia lugha na njia zinazoeleweka kwa kundi husika, ili kuongeza uelewa kuhusu Bima ya Afya kwa Wote na kuhamasisha usajili wa wananchi wengi zaidi.

Kwa upande mwingine, amesema mpango huo pia utazingatia makundi yasiyo na uwezo, yakiwemo wazee, wajawazito na watu wenye ulemavu, ambao wataendelea kupatiwa huduma za matibabu bila malipo kwa mujibu wa utaratibu wa Serikali.

Aidha, ameeleza kuwa katika kuhakikisha taarifa za Bima ya Afya kwa Wote zinamfikia kila mwananchi, Serikali itaingiza ajenda ya bima katika shughuli za kila siku za kijamii na kiuchumi, pamoja na kutumia sanaa, wasanii na teknolojia ya habari katika kampeni za uhamasishaji.

Post a Comment

Previous Post Next Post