Mmiliki wa Kampuni ya Boss Kwezi Limited,George Augustine Kwezi@ B. BOSS KWEZI akiwa Ofisini kwake
Akizungumza na mwandishi Ofisini kwake Kibaha Februari 5,2026 amesema kuwa yeye mpaka hatua aliyofikia na mafanikio aliyonayo sasa alijiwekea malengo pamoja na kutazama fursa ambazo aliona zitamfikisha hatua aliyoipata mpaka sasa katika kampuni yake
Amesema yeye alisoma fani ya ualimu Chuo kikuu Cha Dar es Salaam na kwa mara ya kwanza alipangiwa kufundisha shule ya Sekondari huko Songea .
Baada ya kuona kuwa nimepangiwa huko niliamua kuacha kazi na kurudi Dar es Salaam ambapo niliamua kufundisha shule za private ,lakini nikiwa nafundisha huko nilipata rafiki ambaye alikuwa anauza viwanja na Mimi nikawa namtafutia wateja na alikuwa ananipatia malipo ya laki Moja ,hivyo baada ya kujiwekea malengo Kazi yakufundisha nilifanya Kwa muda baada ya hapo niliamua kuacha kufundisha ndipo tukaungana watu wanne tukanzisha biashara moja kwa kushirikiana na wenzangu ",amesema Boss Kwezi
Aliongeza kuwa tulifanya biashara kwa ushirikiano na baada ya miaka kadhaa kila mmoja kupata mafanikio tuliamua Kila mmoja kujitegemea na ndipo mwaka 2024 nilianzisha kampuni ya Boss kwezi.
"Nina jivunia kwamba mafanikio niliyonayo nimeyapata katika kipindi cha uongozi wa Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan.
"Mafanikio yangu nimeyapata katika kipindi cha Mama Samia kwani amejitahidi kutuacha huru kufanya biashara",amesema Boss Kwezi
Aidha, amesema kwamba katika kampuni ya Boss kwezi Nina miradi mbalimbali na Ofisi zangu zinapatika katika maeneo ya Kibaha ambapo ndio ofisi Kuu,Mbezi,Kinyerezi,Bunju B,Kongowe na Kigamboni.
"Ili ufanikiwe lazima utambue nini unafanya na unapodili na kitu lazima uwe mbunifu sana na Mimi nilikua mwalimu lakini niliona siwezi kufikia malengo yangu nilienda huko kama njia mojawapo ili nikipata fursa niweze kuitumia lakini nilifanikiwa kupata fursa ya kuuza viwanja na niliacha kazi nikiwa bado sijafanikiwa.
Aliendelea kwamba nilipoacha nilifanya Kazi ya kuuza viwanja kwa juhudi sana na ubunifu mkubwa na tunapoenda kununua eneo lazima tulifuatilie Kwa kina na kujua undani wake na hapa yupo mtu maalum ambaye ameajiriwa katika ofisi yangu kwa kazi hii tu ili kuepuka matapeli.
Hata hivyo amesema kazi hii zipo changamoto ambazo usipokuwa makini ya kufuatilia uhalali wa eneo unalotaka kununua unaweza kukumbana nazo na hivyo kazi hii inahitaji umakini wa Hali ya juu sana kwani wapo matapeli ambao wanatamani pesa za Boss kwezi

