Viongozi mbalimbali wa Serikali na Sekta Binafsi, wadau wa Sekta ya Madini pamoja na wageni waalikwa tayari wamewasili katika Hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kushiriki Hafla ya Utiaji Saini wa Mpango Maalum kwa Wachimbaji Wadogo wa Madini kati ya Benki ya CRDB na Tume ya Madini, inayofanyika leo Februari 23, 2026.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo anatarajiwa kuwa Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde (Mb), ambaye anatarajiwa kuongoza tukio hilo muhimu linalolenga kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wachimbaji wadogo wa madini na kuimarisha maendeleo ya Sekta ya Madini nchini.





