MWENYEKITI WA CCM KATA YA BONYOKWA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUWAPELEKEA MAENDELEO

 


Na mwandishi wetu

Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Bonyokwa Vana Kasmiry Mwabena amesema wanajivunia miaka 49 kwa mafanikio makubwa katika Kata yetu kwani tunaona jinsi CCM ilivyo imara

Akizungumza na wanachama wa CCM katika Kata hiyo hivi karibuni Jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 49 ya CCm tangu kuanzishwa kwake amesema tunamshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wote kuanzia Taifa,Mkoa na Kata kuendelea  kukiongoza chama vema kwani matunda yake tunayaona.

"Miaka hii tuna haki ya kujivunia na bado tuko imara,tunaendelea kukienzi chama,kwani Kiko imara hakitikisiki kwa sababu kazi zake ni kubwa na tumeendelea kuziona na tunamshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan lakini pia viongozi wa Chama kuanzia Mwenyekiti wa Chama Taifa,Viongozi wa Mikoa,Wilaya na Kata kuendelea kukitumia chama vema",amesema Mwenyekiti Kasmiry

Aidha,amesema ni mambo mengi na makubwa kwa viongozi wetu wamefanya chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hasas ,nikianza hali ya miundombinu ya Barabara iko vizuri pia tunashukuru tutaendelea kukienzi Chama kwani kinanguvu kubwa na kina msimamo hivyo wanachama tuendelee kuzingatia kanuni na Sheria za chama na kuendelea kukitumikia chama na kukitetea chama Kwa kazi nzuri

Hata hivyo ,amesema ni mambo mengi yamefanyika katika Kata yetu ya Bonyokwa tunajivunia miundombinu ya Barabara,maji,sekta ya elimu zipo shule zimejengwa ,Shule za msingi na Sekondari,tunajivunia kituo Cha Afya kinatoa huduma nzuri kwa wananchi na pia hivi karibuni tumepata ujenzi wa Zahanati.

Ameongeza kwamba maendeleo yaliyofanyika ni mengi sana na haya yote ni matokeo ya uongozi Bora ulioko madarakani.

Aliendelea kwamba katika kata yetu ya Bonyokwa pia tuanajivunia ujenzi wa Kituo cha Polisi ambapo kipo kwenye hatua za mwisho kukamilika.







Post a Comment

Previous Post Next Post