TCRA YAWAPA AHUENI WAANDISHI WA HABARI ZA MITANDAONI

 

Na Angelina Mganga

Dodoma

SERIKALI kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa nafuu ya kutolipa ada ya mwaka mmoja kwa waandishi wa habari wanaoanzisha mitandao ya habari kwa mara ya kwanza ambapo imeelezwa kuwa watajulikana kama 'Amarture online'

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya vya utangazaji February 12,2026 Jijini Dodoma Meneja wa Huduma za Utangazaji wa TCRA,Mhandisi Andrew Kisaka alipokuwa akiwasilisha matokeo na utekelezaji wa mapendekezo yatokayo na utafiti wa huduma za utangazaji nchini wenye kauli mbiu

"Matumizi ya Teknolojia katikq Kupanua na Kuboresha Huduma za Utangazaji Vijijini",

Mhandisi Kisaka amesema kuwa wametoa nafuu hiyo ili kuwapa muda waandishi wa habari wa kujifunza na kupata uzoefu wa uendeshaji wa mitandao ya habari. 

Aidha amesema anayetaka kuanzisha mtandao wa habari alitakiwa alipe ada ya maombi Sh. 50,000 na ada ya leseni sh. 500,000 kwa mwaka.

Hatua hiyo, imepokelewa kwa furaha na wamiliki wa mitandao waliohudhuria mkutano huo ambao baada Mhandisi Kisaka kutangaza walipiga makofi. 

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wa siku mbili ni wanachama wa Mtandao wa Mabloga Tanzania (TBN), Jumuiya ya Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), MOAT, NIBA, Wakongwe RTD, Baraza la Habari Tanzania (MCT), MISA Tanzania na EACO.

Kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, mkutano huo umefunguliwa na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Hamisi Mwinjuma(Mwana FA)









Post a Comment

Previous Post Next Post