Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam
NGOME ya Wanawake ACT-Wazalendo wamejiandaa kuadhimisha siku ya wanawake Duniani kwa kuomboleza kutokana na vifo,ulemavu wa kudumu waliopata wakati wa ghasia zilizofanyika Oktoba 29,2025.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 26,2026 Makao Makuu ya Chama Magome Jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake Janeth Rite amesema hawana sababu ya kusherehekea siku hiyo kwa kufanya sherehe wakati mioyo ya watanzania inamwaga machozi kutokana na kupoteza wapendwa wao na wengine kupata ulemavu wa kudumu mwezi Machi utakuwa ni mwezi wa Maombolezo.
Aidha,amesema siku ya Machi 8,2026 watafanya maombi na hitima pamoja na kutembelea wazee,watoto yatima,kufanya usafi vituo vya afya na kutoa msaada,kuchangia damu,kuzulu makaburi na kufanya mikutano mikubwa ya hadhara nchi nzima.
Pia amesema kauli mbiu Yao ni"Machozi ya Mama ni deni la Taifa",
Rite amesema Ngome ya Wanawake ACT -Wazalendo ni sauti ya wale wasiojiweza kusema na hutuwezi kunyamaza Hadi haki itakapotendeka.
