Na Mwandishi wetu
DAR ES SALAAM
CHAMA cha ACT Wazalendo kupitia Ngome ya Wanawake Leo Machi 3,2026 wamefanya hafla ya uzinduzi wa mnara wa kumbukumbu ya matukio yaliyotokea nchini Oktoba 2025 na siku zolizofuata kwamba Machi ni mwezi wa kukumbuka matukio hayo ya majonzi.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla hiyo Kiongozi wa ACT Wazslendo Dorothy Semu amesema tutatumia mwezi huu kwa maombolezo kwani Tanzania inahitaji uponyaji kutokana na matukio hayo
Naye Naibu Katibu Ngome ya Vijana ACT Wazalendo Taifa Ruquayya Nassir amesema ni vema kutafa namna ya kuponya vidonda vilivyotokana na matukio ya Oktoba ambapo ina hitajika ari kuendeleza mapambano na haki ya uwajibikaji.
Kwa upande wake Mkuu wa Kanisa la Moraviani la Uamsho Tanzania na Afrika Mashariki Askofu Emmaus Mwamakula amesema kuwa matukio yaliyotokea nchini Oktoba 29 ,2025 na siku zilizofuata ni siku za matumaini kutokana na kile alichodai kuwa siku hizo ilikuwa ni mwanzo wa matumaini ya ushindi wa mapambano ya kudai haki nchini.
Amesema kuwa siku hiyo itambuliwe kama siku za matumaini kwa Taifa.
