MULIRO :HATUTAKUBALI JESHI LICHAFUKE KWAWATU WACHACHE

 




Na mwandishi wetu

Dar es Salaam 

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa onyo kali kwa askari wake wanaokiuka maadili kwa kuingilia majukumu ya taasisi nyingine za serikali ili kupata rushwa na maslahi binafsi.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Kanda hiyo SACP Jumanne Muliro Machi 24,2026Jijini Dar es Salaam katika eneo la Raha Square Kariakoo alipotembelea eneo hilo kwa lengo la kufuatilia masuala mbalimbali ya usalama na kuwasikiliza wafanyabiashara.

Amekutana na wadau wa eneo hilo wanaofanya shughuli zao hapo na kuzungumza nao na amesisitiza kwamba askari hawaruhusiwi kisheria kujifanya maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Shirika la Viwango(TBS) .

Aidha,Kamanda SACP Muliro amebainisha kuwa ameshatoa maagizo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala na OCD wa Kariakoo kuhakikisha askari wanabaki kwenye majukumu yao ya msingi ya ulinzi wa raia na mali zao

Amebainisha kuwa polisi jukumu lao ni kufanya uchunguzi na kushirikiana na mamlaka husika na sio kuchukua nafasi za taasisi hizo.

Post a Comment

Previous Post Next Post