MAENDELEO BANK YAENDELEA KUWEKA REKODI YA FAIDA KWA MIAKA 11

 

Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam 

MAENDELEO Bank PLC imeendelea kuweka rekodi ya kipekee kwa kupata faida kwa miaka 11 mfululizo tangu mwaka 2015,inaonesha  uimara wa biashara,uongozi wenye maono na utekelezaji thabiti wa mikakati ya ukuaji endelevu.

Akizungumza na waandishi wa habari Leo Aprili 14,2026 Jijini Dar es Salaam,Mkuu wa Idara ya Fedha Maendeleo Bank PLC ,Nolasco Charles amesema kuwa benki imeendelea kuonesha mafanikio makubwa ya kifedha ,yakithibitisha uwezo wake wa kujua na kuhimili ushindani wa soko.

Aidha amesema kuwa muhtasari wa matokeo ya jumla ya Mapato: TZS 29.05 bilioni, kutoka TZS 23.00 bilioni mwaka 2024 (ukuaji wa 26%)

Amesema Mapato Halisi yatokanayo na Riba: TZS 25.78 bilioni, kutoka TZS 20.06 bilioni (ukuaji wa 28%)

Hata hivyo, amesema Faida Kabla ya Kodi:

 TZS 5.02 bilioni, kutoka TZS 3.85 bilioni (ukuaji wa 30%)

Faida Baada ya Kodi: TZS 4.75 bilioni, kutoka TZS 3.68 bilioni (ukuaji wa 29%) pamoja na 

Uwiano wa Gharama kwa Mapato (CIR): 61.25%

Sambamba na hayo ameeleza kuwa ukuaji huu umechangiwa kwa kiasi kikubwa na kuimarika kwa biashara ya mikopo na kuongezeka kwa imani ya wateja. 

Aliendelea kuwa Kitabu cha mikopo kilikua kwa asilimia 23, huku ubora wake ukiendelea kuimarika kwa kupungua kwa mikopo chechefu hadi asilimia 4.51 kutoka asilimia 4.76 mwaka uliotangulia. 

Sanjari na hayo amesema kuwa Amana za wateja nazo ziliendelea kuongezeka kwa asilimia 31 kutoka TZS 104.02 Bilioni mwaka 2024 hadi TZS 136.20 bilioni mwaka 2025, zikionesha uhusiano imara wa Benki na soko.

 Aidha, jumla ya mali na mtaji wa Benki viliendelea kuimarika, kutoka TZS 104.02 bilioni mwaka 2024 hadi TZS 136.26 bilioni ikiwa ni ukuaji wa 30%. Hali inayoiwezesha Benki katika nafasi nzuri ya kupanua shughuli zake katika kimataifa. Kubwa kuliko zote ni ukuaji wa asilimia zaidi ya mia sita wa thamani ya hisa za benki katika soko la hisa la Dar es Salaam kutoka shilingi 38 mwezi Aprili mwaka 2025 mpaka shilingi 2,480 jana tarehe 13 Aprili , 2026, hii ni imani kubwa sana ya soko kwa Maendeleo Bank.

Ameongeza kuwa Mafanikio haya yamejengwa na utekelezaji madhubuti wa mpango mkakati wa miaka sita 2025 - 2030 (2030 agenda) uliolenga kuimarisha raslimali watu, kuendeleza mageuzi ya kiteknolojia, na kukuza biashara. Benki iliendelea kuweka katika mifumo ya kisasa ya kidigitali, ikiwepo huduma za Mobile Banking na Internet Banking, hatua iliyoongeza ufanisi, kasi ya utoaji huduma, na kuboresha uzoefu wa wateja.

 Benki imeendelea kuweka mkazo katika usimamizi madhubuti wa vihatarishi (risk management), ili kuhakikisha ukuaji wake unaendelea kuwa imara na endelevu.

Aliendelea kwa kusema kuwa  mkakati wa mwaka 2026 itaendelea kumweka mteja mbele katika Kila jambo na benki imejipanga kuendelea kutoa suluhishobunifu,rahisi na Bora kwa wateja ,huku ikiweka kwa vyanzo vya mapato pamoja na kuweka kipaumbele katika mafanikio endelevu.

Alimalizia kwa kutoa shukurani kwa wafanyakazi wote wa Maendeleo Bank PLC kwa kujitolea kwao ,pamoja na wateja wote kuendelea kuiamini benki hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post