MFAHAMU MR CONNECTION

 


Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam 

KIONGOZI wa Pili wa Mila,Tamaduni na Ustaarabu wa mtu Mweusi,Matuta Alkebulani anafahamika kwa jina maarufu la Mr Connection ametoa wito kwa jamii kuwalea watoto katika maadili mema  na malezi Bora kwa kuzingatia haki ya msingi ya  mtoto ya kuishi .

Akizungumza mwandishi wa habari Leo Aprili 22,2026 Ofisini kwake  maeneo ya Kibamba Chama Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam amebainisha kwamba watoto Wana haki ya msingi ya kuishi kwa hiyo yeye ameamua kutoa mali zake na raslimali pamoja nqnkutoa muda wake kwa ajili ya kuwalea na kuwasaidia watoto na vijana wa mtaani ili waweze kufikia ndoto zao.

Amebainisha kwamba takribani miaka kumi sasa tangy ameanza kuwasaidia watoto wa mitaani na mpaka sasa amefikisha idadi ya vijana 80 kupitia kampuni yake ya Mr COnnection .

Aidha ,Kiongozi Matuta @Mr.Connection amewakusanya vijana kwa kuwapatia elimu na ujuzi stadi ikiwemo muziki wa asili huki baadhi ya vijana wanaoendelea na masomo ya elimu ya msingi na sekondari na wengine wakipata mafunzo ya matumizi ta teknolojia.

Mr.Connection ameamua kutoa mali zake na muda wake kwa ajili ya kukaa na watoto na vijana wa mitaani kwani anaamini kwamba watoto wakipewa malezi Bora wanaweza kubadilika hata kama wamepitia changamoto mbalimbali za malezi ya mitaa.

"Watoto wanahaki yakusikilizwa,kuendelezwa na kupewa haki zao za msingi kama binadamu wengine hivi amewaomba wadau na watu wenye mapenzi mema kujitoa kuwasaidia watoto wa mitaani kwani mitaa hailei watoto",amesema

Hata hivyo Mr.Matuta amewata watanzania kuipokea ripoti  ya tume ya uchunguzi wa Oktoba itakayo tolewa Aprili 23,2026 ili maisha yaendelee lakini amesisitiza kuendelea kuienzi amani ya nchi yetu.

Sambamba na hayo, Yeye kama kiongozi amegusia Vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran amesema kuwa Dunia inapitia katika migogoro ya kiuchumi hivyo bi vema ni vema Dunia ikae ili iwe sehemu ya amani

Post a Comment

Previous Post Next Post