MCF na Vodacom watambulisha Afya Mkopo — Mikopo ya Kidijitali Bila Dhamana kwa Biashara za Afya

 




Na mwandishi wetu


PharmAccess kupitia Medical Credit Fund (MCF), kwa ushirikiano na Vodacom Tanzania, imefanya utambulisho wa Afya Mkopo, huduma mpya ya mikopo ya kidijitali bila dhamana kwa vituo vya afya, famasia, kliniki, maabara na wauzaji wa vifaa tiba.

Kupitia mfumo wa LIPA NAMBA, watoa huduma watapata mikopo kwa haraka, kwa urahisi na kwa masharti nafuu ili kupanua huduma, kuboresha miundombinu na kukuza biashara.

Akiongea kwenye kikao cha utambulisho jijini Dar es Salaam,

Dkt. Heri Marwa, Mkurugenzi wa Nchi – MCF, alisema Afya Mkopo inaziba pengo la upatikanaji wa fedha nafuu kwa biashara za afya kupitia teknolojia ya kidijitali.

Bi. Delfina Thomas, Mshauri wa Mikopo ya Kidijitali alibainisha kuwa bidhaa hii inatoa uwazi, kasi na urahisi—ikiwawezesha watoa huduma kuwekeza kwa ufanisi.

Naye Meneja wa ripoti na mipango wa Vodacom Tanzania, Bi. Hellen Kombo  alisisitiza mchango wa LIPA NAMBA katika kukuza ujumuishaji wa kifedha na maendeleo ya sekta ya afya.

Post a Comment

Previous Post Next Post