Na mwandishi wetu
MWENYEKITI wa Chama Cha Tanzania Labour Party (TLP),Richard Lyimo, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa hotuba yake iliyojaa hekima na weledi aliyoitoa mbele ya wazee wa Dar es Salaam. Lyimo amesema hotuba hiyo imeonyesha uwazi, ufasaha na dhamira ya dhati ya kulinda amani na utulivu wa Taifa.
“Hakuna kiongozi anayetamani wananchi wake wapate shida au mashaka. Kila kiongozi mwenye busara hutaka kuona watu wake wakiishi kwa furaha, upendo, amani na umoja,” amesema Lyimo
Lyimo amesema ni muhimu kwa wananchi kuheshimu maagizo na mamlaka zilizopo kwa manufaa ya Taifa.
Aidha, Lyimo aliwataka wazee kuzungumza na watoto na wajukuu wao ili kuhakikisha hawaingii katika vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani ya nchi.
"Nawaomba wananchi tarehe 9 Disemba watulie nyumbani na kuendelea na shughuli zao kama kawaida na kiwataka vijana kuachana mihemko ",alisema
Pia amewataka viongozi wa dini kuepuka kufanya siasa madhabahuni na badala yake wawafundishe waumini maadili mema pamoja na kukaa katika misingi ya dini zetu,viongozi wadini wameitwa na Mungu kuhubiri amani .
Sanjari na hayo amesema kuhusu katiba mpya hili ni suala ambalo limezungumzwa kwa muda mrefu na huu ndio muda muafaka wakulifanyia kazi ili katiba hiyo iendane na matarajio ya wananchi.
