Na mwandishi wetu
DIWANI Kata ya Buyuni Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mhe.Jesca Mahmoud Msolla amesema atahakikisha anashirikiana na Mstahiki Meya wa Jiji hilo Nurdin Bilali Juma na Naibu wake John Mrema pamoja na watendaji wa Halmashauri ya Jiji katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Kata ya Buyuni kwa kipindi chake cha miaka mitano ya uongozi wake.
Ameyabainisha hayo Leo Desemba 4,2025 wakati akizungumza na wanahabari mara baada ya kuapishwa rasmi,huku akitoa ahadi ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa Kata yake iikiwemo elimu,miundombinu ya Barabara,Afya,Maji pamoja na huduma mbalimbali za kijamii
Aliongeza kwamba wananchi wa Kata ya Buyuni hawajakosea kunichagua kuwa diwani wao naahidi kushirikiana nao kwa kila hatua kwani nimejipanga vizuri kuhakikisha natatua kero za wananchi ili kuwaletea mmaendeleo na kutimiza malengo ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
"Nitahakikisha Nina waletea maendeleo wananchi wa Kata yangu ya Buyuni na kufanikisha malengo ya Ilani ya CCM",alisema Mhe.Jesca
Pia amesema kwamba Leo tumemchagua Mstahiki Meya,Nurdin Bilali Juma na Naibu wake John Mrema na sisi Leo tumeapishwa rasmi hii ni hatua ya kuanza kushiriki vikao vya Baraza la Madiwani kwa ajili ya kuwatumikia wananchi katika kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo
