Na mwandishi wetu
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mhe. Bakari Shingo, ametangaza kuwa yupo tayari kushirikiana kwa karibu na Baraza la Madiwani pamoja na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Nurdin Bilali, katika kuhakikisha wananchi wa Jiji la Ilala wanahudumiwa ipasavyo.
Akizungumza leo Desemba 4, 2025, jijini Dar es Salaam wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kilicholenga kumchagua Meya wa Jiji, Mhe. Shingo alieleza dhamira yake ya kushirikiana na viongozi hao katika kuleta maendeleo kwa wananchi. Alisisitiza kuwa ushirikiano huo utaleta tija katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na utoaji wa huduma bora kwa jamii.
Katika hatua nyingine, Mhe. Shingo alieleza kuwa yupo tayari kuwasaidia vijana wa jimbo lake kwa kuwapatia mafunzo ya udereva wa bajaji na bodaboda. Alibainisha kuwa tayari amezindua rasmi mafunzo hayo mnamo Desemba 3, 2025, ambapo zaidi ya vijana 140 wameanza kupata mafunzo hayo katika awamu ya kwanza.
“Pia nategemea kutoa mafunzo kwa gharama za mbunge na mfuko wa mbunge. Vijana wetu walioko katika jimbo letu, kwa wale wasiokuwa na leseni, tunahakikisha wanapatiwa leseni, na kwa wasiojua kabisa, tunawapatia mafunzo. Lengo ni kuwafikia vijana kati ya 600 hadi 800,” alisema Mhe. Shingo.
Aidha, Mhe. Shingo alimpongeza Mstahiki Meya mpya wa Jiji la Dar es Salaam, Nurdin Bilali, kwa kupata kura 48 za ndiyo kati ya kura 51 zilizopigwa, huku Naibu Meya, John Mrema, akipata kura 49 za ndiyo. Kura moja iliharibika katika mchakato huo wa uchaguzi.Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mhe. Bakari Shingo, ametangaza kuwa yupo tayari kushirikiana kwa karibu na Baraza la Madiwani pamoja na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Nurdin Bilali, katika kuhakikisha wananchi wa Jiji la Ilala wanahudumiwa ipasavyo.
Akizungumza leo Desemba 4, 2025, jijini Dar es Salaam wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kilicholenga kumchagua Meya wa Jiji, Mhe. Shingo alieleza dhamira yake ya kushirikiana na viongozi hao katika kuleta maendeleo kwa wananchi. Alisisitiza kuwa ushirikiano huo utaleta tija katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na utoaji wa huduma bora kwa jamii.
Katika hatua nyingine, Mhe. Shingo alieleza kuwa yupo tayari kuwasaidia vijana wa jimbo lake kwa kuwapatia mafunzo ya udereva wa bajaji na bodaboda. Alibainisha kuwa tayari amezindua rasmi mafunzo hayo mnamo Desemba 3, 2025, ambapo zaidi ya vijana 140 wameanza kupata mafunzo hayo katika awamu ya kwanza.
“Pia nategemea kutoa mafunzo kwa gharama za mbunge na mfuko wa mbunge. Vijana wetu walioko katika jimbo letu, kwa wale wasiokuwa na leseni, tunahakikisha wanapatiwa leseni, na kwa wasiojua kabisa, tunawapatia mafunzo. Lengo ni kuwafikia vijana kati ya 600 hadi 800,” alisema Mhe. Shingo.
Aidha, Mhe. Shingo alimpongeza Mstahiki Meya mpya wa Jiji la Dar es Salaam, Nurdin Bilali, kwa kupata kura 48 za ndiyo kati ya kura 51 zilizopigwa, huku Naibu Meya, John Mrema, akipata kura 49 za ndiyo. Kura moja iliharibika katika mchakato huo wa uchaguzi.