SERIKALI KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI ILI KUKUZA UWEKEZAJI NA KUONGEZA AJIRA

 





Na mwandishi wetu

DAR ES SALAAM 

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, amesema Serikali inaelekea kuacha uchumi wa rasilimali asilia na kujikita kwenye uzalishaji, uongezaji thamani na ushindani wa kimataifa ili kufikia lengo la uchumi wa dola trilioni 1 ifikapo 2050.

Akizungumza TNCC, Kapinga amesisitiza ushirikiano wa karibu kati ya Serikali na sekta binafsi kama nguzo ya kukuza viwanda, kuvutia uwekezaji na kuongeza ajira.

Naye Rais wa TNCC, Bw. Vicent Minja, amesema chemba hiyo itaendelea kuwa jukwaa muhimu la wafanyabiashara na mshirika wa Serikali katika maendeleo ya taifa. Ushirikiano Serikali na sekta binafsi waendelea kuimarika kwa uchumi imara na shindani.

Post a Comment

Previous Post Next Post