Na mwandishi wetu
MWENYEKITI wa Chama Cha Makini Taifa, Coaster Kibonde amewatakia watanzania wote kusherehekea kwa amani na upendo pamoja na kudumisha mshikamano katika sherehe za Christmas na Mwaka Mpya
Akizungumza na mwandishi Leo Desemba 22,2025 kwa mahojiano maalum yaliyofanyika kwa njia ya simu amesisitiza amani,upendo pamoja na mshikamano ili amani ya nchi iendelee kutamalaki kwani ndio tunu ya nchi yetu.
"Sikukuu ya Krismas inatukumbusha kuzaliwa kwa mwokozi wetu Yesu Kristo,hivyo tunaposherehekea siku hii muhimu lazima tukumbushane kulinda amani na umoja wetu wa Kitaifa", amesema Mwenyekiti Kibonde
Aidha,Kibonde amesema kwa upande wa Serikali waendelee kuimarisha ulinzi na usalama Kwa raia na Mali zake pia amewataka watanzania waendelee kuwapuuza wanaoleta sitofahamu kwenye mitandao ya kijamii,"tunachohitaji watanzania ni kuwa na amani na utulivu katika nchi yetu ili tuendelee kukuza uchumi wa nchi yetu na mwananchi mmoja mmoja",alisema
Kibonde amewasisitiza vijana kuendelea kuwa wazalendo wa nchi Yao kwani wameundiwa wizara ambayo watapeleka changamoto zao kwa hiyo wawe wastahimivu kwani matatizo Yao yatapata ufumbuzi na wataenda kunufaika na raslimali za nchi
