MWENYEKITI KHATIBU AISIHI JAMII KULINDA AMANI NA MSHIKANO WA NCHI YETU

 

Na mwandishi wetu

MWENYEKITI wa Chama cha ADA-TADEA Taifa, Juma Ali Khatibu ameisihi jamii kuendelea kuitunza amani na utulivu wa nchi yetu hasa katika kipindi hiki tunapoelekea kusherehekea sikukuu ya Christmas na Mwaka Mpya.

Akizungumza na mwandishi Leo Desemba 22,2025 kwa njia ya simu,Mwenyekiti Khatibu amewataka watanzania kudumisha amani  pamoja na kushikamana kuungana kwa  pamoja katika sherehe za Christmas .

"Niwaombe kushikamana na kuungana kwa pamoja katika sherehe za Christmas na Mwaka mpya kwa kuzingatia amani hakuna jambo jema kama kulinda amani  yetu",alisema Khatibu

Aidha,amewaomba vijana wasishawishike Wala kukubali kutumiwa vibaya katika kuleta fujo na vurugu kwa Taifa letu,"Taifa  hili ni la watanzania wote na Serikali imefanya kazi kubwa ya kujenga miundombinu imara na wezeshi kwa ajili ya watanzania wote,niwakumbushe vijana kila kitu kilichojengwa ni Kodi ya watanzania kwahiyo tulinde miundombinu yetu",alisisitiza.

Pia amewataka vijana kudumisha amanii na utulivu waache kisikiliza habari za mitandao ,wasa wale wanaotumiwa vibaya na na baadhi ya mataifa 

Hata hivyo ,amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kati ya baadhi ya hotuba yake mojawapo ailyoitoa kwamba Kazi ya vyombo vyq ulinzi na Usalama ni kuwalinda watanzania na Mali zao kwa hiyo tunawatakia wakristo wote duniani kote kusherehekea Christmas  kwa amani

Post a Comment

Previous Post Next Post