KATA YA KISUKURU KWA SIKU 100 ZA RAIS YAWEKA MKAKATI WA KUFUTA UFAULU WA "DIVISION ZERO"


Na mwandishi wetu

Dar es Salaam 

KATIKA kipindi cha siku 100 za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Kata ya Kisukuru iliyopo Jijini Dar es Salaam imekuja na mpango mkakati wa kutokomeza ufaulu wa daraja sifuri( division zero) katika sekta ya elimi ili kuongeza ufaulu  wa wanafunzi katika shule za serikali.

Hayo yamebainishwa na Diwani wa Kata ya Kisukuru ,Mhe.Lucy Lugome wakati akizungumza na waandishi wa habari,amesema Kata hiyo Ina shule ya msingi moja ambayo ni Magoza na sekondari Moja ya Magoza,mkakati huo umeanza kutekelezwa kwa shule ya sekondari kwa wanafunzi wa kidatocha nne.

Diwani Lugome amesema kwamba baada ya kupitia matokeo ya miaka Miya iliyopita ,alibaini ufaulu unapanda na kushuka,Hali inayopelekea kutumia siku 100 za Rais kuweka mkakati madhubuti ya kuboresha matokeo,ikiwemo kupunguzq division four na kuongeza ufaulu.

"Mkakati wa utekelezaji umeanza kwa kuitisha vikao vya pamoja kati ya walinu na wazazi wa wanafunzi wa kidato Cha pili na Cha nne,aidha amesema atagharimia  mitahani yote itakayofanyika ili kufuatilia maendeleo ya wanafunzi na kuwajengea Ari ya kufanya vizuri",alisisitiza 

Aloendelea kuwa walimu wameqnza kufanya tathimini ya matokeo ya Kila mwezi Kwa wanafunzi wa kidato Cha pili na Cha nne,hatuw inayolenga kuwajengea wanafunzi kujiaminj na kujiandaa vema kwa mitihani ya Taifa.

,"Tumejipanga kukabilianana changamoto ya utoro shuleni kwa kushirikiana na Jeshi la Olisi kufanya doria na kutoa elimu kwa wanafunzi

Ameongeza kwamba Kata ya Kisukuru imefanikiwa kupata jengo halali la serikali kwa ajili ya ofisi za kata,baada ya awali kutumia jengo la kupanga,Hali itakayoongeza ufaniasi wa utendaji Kazi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Mikopo ya asilia 10,amesema mwaka 2017 kulikuwa na changamota za urejeshaji kwa Sasa baraza la kata limeanza kujadili mikakati ya kuhakikisha  vinana wanawake na wenye ulema u wananufaika zaidi.

"Baadhi ya vikundj vya vijana wa bodaboda vimepata mikopo nda I ya siku 100 za Rais Samia ,alisisitiza kuwa juhudi zinaendelea kuhakikisha mikopo hiyo inawafikia wajasiriamali wadogo wakiwemo akinamama na vijana ili kuleta tija kwa wananchi",amesema

Katika sekta ya Afya,Lugome amesma wanamshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha ujenzi wa hospitali ya ghorofa tati itakayogharimu shilingi bilioni tank,ambapo taratibu zote za awali zimekamilika.

Aidha,amesema ujenzi wa hospitali hiyo unatarajiwa kuanza rasmi katika awamu hii ya uongozi 2025/2030 hatua itakayoboresha upatiknaji wa huduma za afya kwa wakazi wa Kata ya Kisukuru na maeneo ya jirani.

Post a Comment

Previous Post Next Post