Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Temeke imefanikiwa kuokoa jumla ya shilingi 2,699,927,611 zilizokusanywa kutoka kwa waajiri mbalimbali wa sekta ya binafsi waliokuwa wakidaiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) Temeke pamoja na kupokea malalamiko 48 ,ambapo malalamuki 22 yaliyohusu tuhuma za rushwa na yamefanyiwa kazi na yapo katika hatua za uchunguzi na malalamiki 26 yamefikishwa katika idara husuka.
Akizungumza na waandishi wa Habari Leo Machi 5,2026 Jijini Dar es Salaam Naibu Mkuu wa TAKUKURU(M) Temeke ,Ismail Bukuku amewahiza wananchi wa Wilaya ya Temeke na Kigamboni kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya rushwa.
"Vita hii si ya taasisi Moja pekee ,bali ni jukumu la Kila mmoja wetu.Ni kwa mshikamano,ujasiri na uwajibikaji wa pamoja ndipo tutaweza kujenga Tanzania yenye haki,uadilifu na maendeleo ya kweli,Tanzania isiyokuwa na rushwa",amesema
Aidha ,amesema katika kipindi Cha Oktoba Hadi Disemba 2025 TAKUKURU Mkoa wa Temeke imefanikisha kumfikisha mahakamani Askofu Renatus Joseph Nyalalikuto wa Kanisa la Hosanna Assemblies Of God Tanzania(HAOGT) kwa tuhuma za kughushi nyaraka na kutoa nyaraka za uongo zinazohusiana na umiliki wa ardhi ili aweze kujipatia kiwanja chenye thamani ya shilingi 60,000,000/=
Hata hivyo,Naibu Mkuu wa Takukuru(M) Temeke ,Ismail Bukuku amesema uchunguzi wa kina uliofanywa na TAKUKURU baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mmoja wa warithi na msimamizi wa mirathi ya marehemu Ally Hamad Hillal.
"Kutokana na ushahidi uliokusanywa na kufanywa na kufanyiwa uchambuzi wa kitaalamu,TAKUKURU imefungus Kesi ya jinai CC/26097/2025 dhidi ya Askofu Renatus Joseph Nyalali,katika Mahakama ya Wilaya ya Kigamboni",amesema
Ameongeza kuwa kwa mujibu wa hati ya mashtaka,imedaiwa kuwa katika kiindi cha mwaka 2021 hadi 2022,mshtaka alighushi nyaraka sahihi za wanafamilia wa marehemu kwa lengo la kujipatia umiliki wa eneo la ardhi lililopo Mtaa wa Kizani Geza Ulole,Wilaya ya Kigamboni.Eneo Hilo lilinunuliwa mwaka 2008 kwa kiasi cha shilingi milioni sitini na kuachwa kama urithi kwa watoto wa marehemu.
"Imedaiwa pia,Mshtakiwa alitumia mwanya wa kuaminiiwa na familia ya marehemu kuandaa nyaraka za uwakilishi(Power of Attorney) kwa njia isiyo halali.Nyaraka hizo zilidaiwa kutumika kupima eneo hilo na kuligawa katika viwanja tisa,ambavyo baadaye vilikuwa vikiuzwa kwa watu mbalimbali kwa kutumia majina na sahihi za kughushi za wanafamilia.Aidha,uchunguzi umebaini kuwa katika baadhi ya viwanja hivyo,mtuhumiwa alijiorodhesha mwenyewe kama mmiliki halali", amesisitiza
Pia amebainisha kwamba uchunguzi huo ulifanywa kwa kushirikiana na mamlaka za usimamizi wa ardhi kwa kuzingatia vifungu vya 333,335(a) na 337 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu vinavyohusu makosa ya kughushi,pamoja na kifungu Cha 342 kinachohusu uwasilishaji wa nyaraka za uongo.
Sambamba na hayo ,amesema kuwa TAKUKURU itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa mijibu wa Sheria kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola na kuendelea kuchukua hatua stahiki dhidi ya vitendo vya rushwa,udanganyifu na uhalifu wa aina yoyote bila kuzingatia hadhi au nafasi ya mhusika,kwa lengo la kulinda maslahi ya umma na misingi ya haki.
Sanjari na hayo,TAKUKURU imeendelea kufuatilia matumizi ya fedha na utekelezaji wa miradi 2 ya maendeleo hivyo ushauri uliotolewa na kufuatia dosari zilizobainishwa umetekelezwa na wahusika kwa wakati kwa hiyo imesaidia kurekebisha mapungufu na kuimarisha usimamizi wa raslimali za umma pamoja na kuongeza uwazi,uwajibikaji na thamani ya fedha katika miradi
Ameendelea kwa kusema kuwa TAKUKURU Mkoa wa Temeke ilifuatilia matumizi ya jumla ya shilingi 36,532,990,529 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 4 ya maendeleo katika sekta ya elimu,afya na ujenzi inayotekelezwa na Halmashauri za Manispaa ya Temeke na Kigamboni.
Katika kipindi chote wamefanikiwa kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu madhara ya rushwa,haki na wajibu katika kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa pamoja na taratibu sahihi zakutoa taarifa,pia kuimarisha ushirikiano kati ya wananchi na taasisi katika utoaji wa taarifa za vitendo vya rushwa kwa asilimia 50 ikilinganishwa na robo iliyopita.
"Mafanikio hayo yalitokana na utoaji wa elimu kwa wananchi 404,804 kupitia mikutano 12 ,maonesho 4 ,semina 35,uimarishaji wa klaby 11 za wapinga rushwa katika shule za msingi,sekondari na vyuo pamoja na vipindi 12 vya redio na televisheni",alisema
Amebainisha kwamba kesi 2 zilifunguliwa Mahakamanj,kesi 2 Jamhuri imeshinda ba kesi 8 zinaendelea Mahakamani
TAKUKURU Mkoa wa Temeke imejipanga kutekeleza mikakati ya robo ya Januari Hadi Machi 2026 kwa kuandaa na kutekeleza bonanza kubwa la wanafunzi wa shule za sekondari wanaoshiriki katika klabu za wapinga rushwa zilizopo Wilaya ya Temeke likijumuishq michezo,nyimbo,mashairi,maigizo na mada mahsusi kwa lengo la kuimarisha uelewa na ushiriki wa vijana katika mapambano dhidi ya rushwa.
Alimalizia kwa kutoa wito kwa wananchi kujiepusha kabisa na vitendo vya rushwa na kuchukua hatua za kijasiri kwa kutoa taarifa pale wanapobaini dalili za rushwa katika maeneo yao
